Home International LIVERPOOL MWENDO WAKE MGUMU

LIVERPOOL MWENDO WAKE MGUMU

LICHA ya kuwa na mastaa wake wote ndani ya kikosi cha Liverpool ikiwa ni Mohamed Salah, Roberto Firmino, Virgil Van Djik waliambulia pointi moja mbele ya Everton kwenye Merseyside Dabi.

Unakuwa ni mchezo wa tatu kwa Liverpool kupata sare msimu huu ikiwa imecheza mechi sita, imeshinda mbili na ilinyooshwa mbele ya Manchester United jambo linaloonesha kuwa mwendo wake msimu huu ni mgumu.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Goodison, Everton bao lao ambalo walifunga kwenye mchezo huo lilifutwa baada ya teknolojia ya VAR kueleza kuwa ilikuwa ni bao la kuotea.

Jumla yalipigwa mashuti 37 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Matokeo hayo yanafanya Liverpool kufikisha pointi 9 nafasi ya 6 huku Everton wakifikisha pointi nne nafasi ya 16

Previous articleVIDEO:MWAKINYO ABAINISHA ALIIBIWA BEGI
Next articleVIDEO:ISSA AZAM WA ASEMA MAYELE ALIOMBA KUCHEZA SIMBA