Home Uncategorized MSAFARA WA SIMBA KUREJEA DAR

MSAFARA WA SIMBA KUREJEA DAR

BAADA ya kumaliza kazi kwenye mechi mbili za kirafiki ambazo walialikwa nchini Sudan na Klabu ya Al Hilal, kikosi cha Simba leo Septemba Mosi kinatarajiwa kurejea Dar.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki iliweza kupata matokeo kwenye mchezo mmoja chanya na mwingine waliweza kupata matokeo hasi.

 Kwenye mchezo wa kwanza walipata ushindi wa mabao 4-2 Asante Kotoko na ule wa pili kilinyooshwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Al Hilal.

Kipa ambaye aliweza kupata nafasi kwenye mechi hizo za kimataifa alikuwa ni Ally Salim ambaye hakuwa na nafasi kwenye mechi za mwanzo.

Makipa wawili wa Simba ambao ni Aishi Manula na Beno Kakolanya majina yao yapo kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayofanya maandalizi kuikabili Uganda, Septemba 3 mchezo wa marudio kufuzu CHAN.

Pia kiungo Sadio Kanoute raia wa Mali alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye mashindani hayo baada ya kukosekana kwenye mchezo wa kwanza alipokuwa na ruhusa maalumu.

Previous articleVIDEO:MZEE MCHACHU AMVAA KOCHA WA SIMBA
Next articleANFIELD LIVERPOOL YABAKI NA POINTI ZOTE TATU