Home Sports YUSUPH MHILU WA SIMBA ASAINI KAGERA SUGAR

YUSUPH MHILU WA SIMBA ASAINI KAGERA SUGAR

MSHAMBULIAJI Yusuph Mhilu amepewa dili la mwaka mmoja kuweza kuitumikia Klabu ya Kagera Sugar.

Ni mwaka mmoja ameweza kusaini kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara na inatumia Uwanja wa Kaitaba.

Atakuwa hapo kwa mkopo kwa kuwa alisaini dili la miaka mitatu Simba na ametumia mwaka mmoja.

Msimu uliopita wa 2021/22 hakuwa chaguo la kwanza ndani ya Simba chini ya Kocha Didier Gomes,Franco Pablo jambo lililofanya rekodi zake kuwa za kawaida.

Hakuweza kufunga bao ndani ya ligi kwenye mechi ambazo alicheza ndani ya kikosi cha Simba ambacho kilimaliza msimu kikiwa nafasi ya pili.

Previous articleUWANJA WA MKAPA MAMBO NI BYUTIBYUTI
Next articleBM 33:NIMERUDI JAMANI,AOMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI