Home Sports BM 33:NIMERUDI JAMANI,AOMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI

BM 33:NIMERUDI JAMANI,AOMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI

KIUNGO wa Yanga, Bernard Morrison ambaye amerejea katika kikosi hicho kwa kusaini dili la miaka miwili ameweka wazi kuwa anahitaji msamaha kwa yale ambayo aliyafanya na sasa amerejea.

Jina la kiungo huyo lilipotajwa aliingia uwanjani huku akisema nimerudi,nimerudi jamani.

Nyota huyo alitambulishwa kwa mara ya kwanza na Yanga kabla ya kusaini dili la miaka miwili Simba na msimu wa 2021/22 ulikuwa ni wa mwisho kuitumikia Simba.

Amerejea Yanga akiwa ni mchezaji huru kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umegota ukingoni.

Ametambulishwa na Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Yanga na kuomba apewe dk 10 za kuongea mbele ya mashabiki wengi na viongozi ambao wamejitokeza Uwanja wa Mkapa.

“Ninaweza kusema kwamba ninaomba msamaha kwa yale ambayo yametokea na sasa nimerudi ndani ya Yanga baada ya kuwa nje ya hapa kwa muda.

“Ambacho nina amini nipo sehemu salama na tuna kocha mzuri ambaye ni kocha bora Afrika hivyo yale yote yaliyofanyika msimu uliopita tutaendelea nayo,” amesema.

Yanga itahitimisha Wiki ya Mwananchi kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Vipers SC ya Uganda ambayo anacheza Censor Manzoki mshambuliaji anayetajwa kumalizana na Simba.

Previous articleYUSUPH MHILU WA SIMBA ASAINI KAGERA SUGAR
Next articleYANGA YAAMBULIA KICHAPO MBELE YA VIPERS SC