Home Sports UWANJA WA MKAPA MAMBO NI BYUTIBYUTI

UWANJA WA MKAPA MAMBO NI BYUTIBYUTI

UWANJA wa Mkapa mambo ni byutibyuti,mashabiki wa Yanga baadhi tayari wapo ndani ya uwanja kusubiri burudani na utambulisho wa wachezaji wapya huku mambo yakiwa ni byutibyuti.

Mbali na utambulisho huo pia kuna mechi ya kimataifa ya kirafiki ambayo inatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku itakuwa dhidi ya Vipers SC.

Mgeni rasmi wa shughuli ya leo ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (Bara), Abdulrahman Kinana.

Tayari mashabiki wa Yanga wameanza kuwasili uwanjani ilikuwa ni kuanzia majira ya saa 1:00 asubuhi huku baadhi ya tiketi zikiwa tayari zimeisha kuanzia ile ya VIP na VIP A.

Nyota wa Yanga,Bernard Morrison amesema kuwa ni muhimu kwa mashabiki kuweza kujitokeza kwa wingi kuona namna hali itakavyokuwa.

“Jamani jamani njooni kwa wingi jamani,tupo vizuri na tunajua kwamba kuna mambo mengi ambayo tumeyaandaa kwa ajili yenu,”.

Pia Kocha Mkuu wa Yanga,Nasreddine Nabi amesema kuwa wakati wa Yanga kushuhudia burudani ni leo.

“Ni muda wa kushuhudia burudani kutoka kwa wachezaji pamoja na maandalizi ambayo tumeyafanya mashabiki jitokezeni kwa wingi,” .

Previous articleBEACH SOCCER TIMU YA TAIFA KAZI NI KESHO
Next articleYUSUPH MHILU WA SIMBA ASAINI KAGERA SUGAR