Home Sports BEACH SOCCER TIMU YA TAIFA KAZI NI KESHO

BEACH SOCCER TIMU YA TAIFA KAZI NI KESHO

HATIMAYE kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ‘Beach Soccer’ ambacho kinajiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu AFCON (BSAFCON) dhidi ya Malawi utakaofanyika kesho Agosti 7, 2022, yameendelea kufunga hesabu yake ya maandalizi hayo kwenye Fukwe za Coco jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya mwishomwisho yaliyofanyika jana Ijumaa Agosti 5  na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidau, yalionekana kuwa na hamasa kubwa kiasi cha kila aliyeshuhudia kuondoka na matumaini ya kesho kupata ushindi mnono.

Kocha wa kikosi hicho, Boniface Pawasa kwa kushirikiana na Kocha wa Mkuu wa Timu ya Taifa ya Oman, Talib Hilal, walionekana wakifundisha zaidi mbinu za ufungaji jambo linaloashiria wawili hao kuhitaji ushindi mnono mbele ya Malawi.

Kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu katika michuano hiyo, uliopigwa nchini Malawi, timu hiyo ilipoteza dhidi ya Malawi kwa kupigwa mabao 3-2, jambo ambalo limewafanya kuongeza juhudi za mazoezi ili waweze kupata ushindi mnono nyumbani na kujitengenezea nafasi ya kuendelea katika hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Previous articleMAKOCHA SIMBA NA YANGA KUIBIANA MBINU KWA MKAPA
Next articleUWANJA WA MKAPA MAMBO NI BYUTIBYUTI