Home Uncategorized YANGA WATAJA SABABU YA KUMPA MKATABA AZIZ KI

YANGA WATAJA SABABU YA KUMPA MKATABA AZIZ KI

BAADA ya kukamilisha utambulisho wa kiungo wa Yanga, Aziz KI uongozi wa Yanga umetaja sababu ya kumsajili kiungo huyo kuwa ni uwezo wake.

Inaelezwa kuwa usajili wa kiungo huyo aliyekuwa anakipiga ndani ya ASEC Mimosas umewatoa Yanga milioni 700 akiwa amepewa kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia mabingwa mara 28 wa Ligi Kuu Bara.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ni moja ya usajili mzuri ambao utakuwa na matokeo chanya kwa timu hiyo kwenye ligi na mashindano ya kimataifa.

“Usajili wa Aziz KI umekamilka na sasa mashabiki wameshajua kwamba tulikuwa tunamaanisha kwamba kutakuwa na vitu vizuri kwa ajili yao na sababu ya kumsajili ni uwezo wake.

“Uwezo wake ni sababu kubwa ya sisi kuweza kumsajili kwani hakuna ambacho kimetufanya tumsajili zaidi ya jambo hilo,tunataka kufanya vizuri kitaifa na kimataifa hivyo ni lazima tuwe na wachezaji wenye uwezo kama ilivyo kwa Aziz KI,”

Nyota huyo alikuwa anatajwa kuingia rada za Simba na Azam FC ambao walikuwa wanahitaji kupata saini yake mwisho ametambulishwa Yanga.

Ilikuwa ni usiku wa manane nyota huyo alitambulishwa baada ya usajili wake kukamilika.

Previous articleVIDEO:OKRA AMEANZA KWA KUTUPIA,AZUNGUMZA KWA FURAHA
Next articleAZAM FC YATAMBIA USAJILI WAO