Home Sports BURUNDI KUCHEZA NA CAMEROON UWANJA WA MKAPA

BURUNDI KUCHEZA NA CAMEROON UWANJA WA MKAPA

TIMU ya Taifa ya Burundi inatarajia kukabiliana na Timu ya Taifa ya Cameroon katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Juni 9,2022.

Kuelekea mchezo huo, Shirikisho la Soka la Burundi kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu, Riziki Jacob limeishukuru Tanzania kwa kuikaribisha timu hiyo pamoja na ukarimu walioupata kutoka kwa wadhamini wao Kampuni ya GSM.

Riziki ameanza kwa kuongelea historia ya undugu na ushirikiano baina ya Tanzania na Burundi tangu wakati wa ukoloni ambapo amebainisha kuwa Tanzania na Burundi ni ndugu kwani wamefanikiwa kushirikiana katika Nyanja zote ikiwemo siasa na ukombozi wa nchi zao.

“Katika masuala ya ushirikiano hatuna tatizo kwa kuwa Tanzania na Burundi ni ndugu hivyo tumekuja hapa ili kuweza kuimarisha undugu wetu ambao upo kwa muda mrefu, mashabiki Watanzania na Warundi wajitokeze kwa wingi,”.

 Haji Manara ambaye ni Mtanzania,ameteuliwa na Shirikisho la Soka Burundi kuwa mhamasishaji katika tukio hilo muhimu kwa historia ya nchi ya Burundi.

 Manara amesema anawaomba Watanzania pamoja na Warundi wote wanaoishi nchini Tanzania wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu ya Taifa ya Burundi katika pambano lake dhidi ya Cameroon.

“Uwanja wa Mkapa tutashuhudia mchezo mkubwa na wenye ushindani mkubwa kwa sasa ni kuona kila mmoja anajitokeza hasa ukizingatia kwamba viingilio ni 2000 na 5,000 VIP B na A ni 10,000,”.

Previous articleKAZI INAENDELEA KWA TIMU ZA TAIFA,MUHIMU MIPANGO
Next articleKUMUONA GEORGE MPOLE,SAMATTA BUKU 3