Home Sports KUMUONA GEORGE MPOLE,SAMATTA BUKU 3

KUMUONA GEORGE MPOLE,SAMATTA BUKU 3

 BAADA ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Niger nchini Benin sasa hesabu za timu ya Taifa ya Tanzania ni kuelekea kwenye mchezo ujao dhidi ya Algeria unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 8, mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani huu ni mchezo muhimu kwetu na ushindi wetu ni furaha kwa kila mmoja huku malengo yakiwa ni Kufuzu Afcon.

Kiingilio ni bei rafiki kwenye mchezo huo amapo ni 5,000 kwa VIP na 3,000 kwenye mzunguko.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF), Cliford Ndimbo amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri kwa wachezaji kuendelea na mazoezi mara baada ya kurudi kwenye mchezo wao dhidi ya Niger.

“Malengo yetu ni kuweza Kufuzu Afcon kitakachotupa nafasi ya kuweza kuwa hapo ni matokeo mazuri hivyo mchezo wetu dhidi ya Algeria ni muhimu kwetu kupata matokeo.

“Ukiangalia namna ilivyo ushindani ni mkubwa na wapinzani wetu wapo imara ambacho tunaangalia sisi ni kupata ushindi hasa kwa kutegemea nguvu ya mashabiki ambao nao wanamchango mkubwa.

“Uwanja wa Mkapa sera yetu ni kwamba hatoki mtu na hawa wanaokuja tunawaheshimu lakini tunahitaji ushindi kwenye mchezo wetu,kila kitu kinakwenda sawa kwa upande wa wachezaji benchi la ufundi linajua namna ya kufanya na sisi mashabiki basi tujitokeze kwa wingi,” amesema Ndimbo.

Previous articleBURUNDI KUCHEZA NA CAMEROON UWANJA WA MKAPA
Next articleBREAKING:BIASHARA UNITED YAVUNJA BENCHI LA UFUNDI