Home Sports BREAKING:BIASHARA UNITED YAVUNJA BENCHI LA UFUNDI

BREAKING:BIASHARA UNITED YAVUNJA BENCHI LA UFUNDI

RASMI uongozi wa Biashara United umevunj benchi la ufundi kutokana na mwendo mbaya wa timu hiyo.

Ni Vivier Bahati, aliyekuwa Kocha Mkuu wa iashara United pamoja na msaidizi wake.

Ofisa Habari wa Biashara United Salma Thabit amesema kuwa wanatambua mchango ambao wameweza kuongoza kwenye mechi zao.

“Tunajua kwamba benchi la ufundi limekuwa na mchango mkubwa ila kwa sasa tunaangalia namna gani tutaweza kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja,” amesema.

Kwenye msimamo Biashara United ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 24 na mchezo wa mwisho ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Previous articleKUMUONA GEORGE MPOLE,SAMATTA BUKU 3
Next articleVIDEO:HAJI MANARA KUOMBA MBINU KWA SIMBA