Home Sports KAZI INAENDELEA KWA TIMU ZA TAIFA,MUHIMU MIPANGO

KAZI INAENDELEA KWA TIMU ZA TAIFA,MUHIMU MIPANGO

WAMEANZA kwa mwendo mzuri wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars kwenye mchezo wao wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Niger.

Sare ya kufungana bao 1-1 ugenini haina ubaya lakini ni muhimu kuweza kuendelea kuongeza juhudi hasa kwa mechi ambazo zinakuja ili kuweza kufuzu Afcon.

 

Mchezo ujao wachezaji bado wana kazi ya kusaka ushindi ambapo itakuwa dhidi ya Algeria kwenye Uwanja wa Mkapa na sasa tutakuwa nyumbani.

 

Kwa namna ambavyo maandalizi yameanza kwa mara nyingine tena tunaona kwamba kwa mechi zijazo kila kitu kitakuwa sawa na bendera itawakilishwa bila makosa.

 

Inawezekana kupata ushindi hasa kwa kuwa tutakuwa nyumbani na inawezekana kupoteza kwa kuwa na wapinzani nao watakuja na mbinu zao za kusaka ushindi.

 

Kufanya kwa wachezaji vizuri kwenye mechi zilizobaki itakuwa ni sehemu ya kufungua milango ya kufikia mafanikio na kufuzu Afcon hivyo ni wakati wa wachezaji kuweza kufanya kweli.

 

Mashabiki kwa sasa wanapenda kuona kwamba wachezaji wengi wanapata nafasi za kucheza nje ya nchi hilo litazidi kufungua upana wa uzoefu pamoja na kuwa na wachezaji wenye uzoefu kutoka nje ya nchi.

 

Wengi wanapenda kuona mafanikio makubwa kwa wakati huu lakini ni kazi ambayo inahitajika kufanyika kwa kushirikiana kila mmoja.

 

Maumivu ambayo mashabiki wamekuwa wakiyapata kwenye mechi za kimataifa yanatosha na sasa ni muda wa kuweza kuwapa furaha kwa namna yoyote ile.

 

Yapo mengi ambayo yanapaswa kuboreshwa ili kuweza kupiga hatua kubwa zaidi ya hapa na kinachohitajika ni kuweza kuongeza nguvu na wachezaji kujituma bila kuogopa.

 

Pia wakati wa maandalizi ni muhimu wachezaji wakatambua kwamba furaha ya Watanzania imebebwa kwenye miguu yao hivyo wanakazi ya kufanya ili kuwapa furaha mashabiki.

 

Kurejea kwao na kuanza moja kwa moja kambi iwe na manufaa kwa kila mmoja na wachezaji waendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa bidi.

 

Jambo la msingi kwa wachezaji ni kuzingatia maelekezo ya benchi la ufundi na kufanya kile ambacho kitakuwa na faida kwa timu hiyo itafanya matokeo yaweze kupatikana kwa urahisi.

 

Watanzania tuzidi kushirikiana kwa ajili ya kuona mafanikio ya timu yanatuhusu na sisi pia hivyo muda ukifika wa mchezo basi tujitokeze kwa wingi kuweza kuwa nao bega kwa bega kwenye mchezo uwanjani.

 

 

Kujitokeza kwa mashabiki kunaongeza nguvu kwa wachezaji kufurahia uwepo wa wale wanaojitokeza pamoja na kuzidi kujituma zaidi katika kutimiza majukumu yao.

 

Tunajua kwamba Watanzania wanapenda mpira na wanapenda kuona timu zikifanya vizuri hivyo ni muda wa kujitokeza kwa mchezo wa marudio utachezwa Uwanja wa Mkapa.

 

Kila siku kwa wachezaji wanapokuwa uwanjani nao wanajukumu la kuwapa furaha mashabiki wale ambao watakuwa wamejitokeza uwanjani basi muda ni huu wa kuweza kujitokeza.

 

Jambo lawachezaji wakiwa uwanjani ni moja kucheza kwa kushirikiana na kuipa timu matokeo hilo ni muhimu kwa kila mchezaji kujua.

 

Ambacho kitawafanya mashabiki kujitokeza uwanjani ni matokeo mazuri na juhudi za kila mmoja kufanya vizuri kwenye mchezo husika.

Tunaona kwamba wapo mashabiki ambao waliungana na timu iliposafiri kwenda kushangilia katika hilo pongezi mnastahili kwa kuwa hamjafanya jambo dogo hilo ni kubwa kwa kweli.

Kwenye mechi ambazo zitachezwa hapa nyumbani nina amini kwamba wale ambao walikwama kusafiri basi watatumia fursa kujitokeza uwanjani.

Hongereni pia U 17 Serengeti kwa kuweza kufuzu Kombe la Dunia, kaz bado inaendelea.

 
Previous articleMWENDO WA CHICO USHINDI YANGA UPO HIVI
Next articleBURUNDI KUCHEZA NA CAMEROON UWANJA WA MKAPA