MANCHESTER CITY YAIBAMIZA ATLETICO MADRID

WAKIWA Uwanja wa City of Manchester waliweza kupata ushindi wa bao 1-0 Atletico Madrid ikiwa ni mchezo wa UEFA Champions League.

Huu ni mchezo wa kwanza robo fainali na mtupiaji alikuwa ni Kevin De Bruyne ilikuwa dk ya 70.

City iliweza kuwa imara kila idara mwanzo mwisho katika mchezo huo licha ya Atletico Madrid kupaki basi mwanzo mwisho.

Ni mashuti 15 City walipiga langoni mwa Atletico Madrid huku mawili yalilenga lango na 13 yakienda nje ya lango huku wapinzani wao wakishindwa kupiga hata shuti moja kuelekea langoni mwa City.

Ni kona 9 walipiga City na Atletico hawakupata kona hata moja.