LEO Jumapili michuano ya AFCON 2021 inatarajiwa kufika tamati baada ya kuchezwa kwa siku 28 kuanzia Januari 8,2022 huku wengi wakitarajia kuona mchezo mzuri ndani ya dakika 90 nchini Cameroon.
Timu 24 zilianza hatua ya makundi hadi leo zimebaki mbili ambazo zitacheza fainali kusaka bingwa baada ya wenyeji Camroon kupata ushindi kwa penalti mbele ya Burkian Faso kwenye mchezo wa kibabe uliokuwa na ushindani mkubwa.
Ni fainali kati ya Misri yenye Mohamed Salah dhidi ya Senegal yenye Sadio Mane ambao wote wapo ndani ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England.
Salah ni kinara wa utupiaji kwa Misri akiwa ametupia mabao mawili huku Mane akiwa ametupia mabao matatu.
Mpaka inatinga fainali Senegal imefunga mabao tisa na kuruhusu mabao mawili huku Misri ikiwa imeruhusu bao moja kwa muda wa kawaida na ikifunga mabao manne.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)