Home Sports NDEMLA MAMBO MAGUMU MTIBWA SUGAR

NDEMLA MAMBO MAGUMU MTIBWA SUGAR

KIUNGO wa Mtibwa Sugar, Said Ndemla mambo kwake yamekuwa magumu ndani ya Mtibwa Sugar kwa sasa kwa kwa tangu alipofunga bao Desemba 12/2021 mpaka leo hajaweza kufurukuta tena kwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Ndemla upo hapo kwa mkopo ambapo alijiunga na timu hiyo akitokea kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Leo Februari 5 anatimiza siku ya 55 bila kuweza kufunga wala kutoa pasi kwenye timu hiyo inayotumia Uwanja wa Manungu kwa mechi zake za nyumbani.

Mchezo wao ujao ni Februari 6,2022 itakuwa Uwanja wa Ilulu, dhidi ya Namungo FC.

Kwenye msimamo Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 13 ikiwa imecheza mechi 13 imekusanya 12 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 7.

Previous articleSIMBA QUEENS YAPIGA KIFURUSHI CHA WIKI
Next articleMORRISON ATAJWA KUIBUKIA YANGA