>

MASHINE MPYA YANGA YAIPIGIA HESABU SIMBA

IKIWA ni mara ya kwanza amecheza mechi akiwa na Yanga kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni, beki Mzanzibar, Ibrahim Bacca, amesema kuwa amekuja Yanga ili kuweza kutimiza majukumu ya kusaka ubingwa.

Kwa sasa ubingwa wa ligi upo mikononi mwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Bacca amesema kuwa ni fahari kwake kucheza ndani ya Yanga kwa sababu ni timu kubwa na yenye malengo na yeye ujio wake ndani ya timu hiyo, anaamini atasaidiana na wenzake ili kutwaa ubingwa.

Beki huyo wa kazi Bacca amesema yupo kwenye timu yenye malengo na yeye anatakiwa kuwa miongoni mwa malengo hayo na kwa ushirikiano wa Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na walinzi wengine kwenye kuilinda Yanga.

“Nimekuja hapa ili kuweza kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu. Najua hilo litawezekana kwa sababu haya ni malengo ya timu yetu.

“Kwa ushirikiano wa kina Mwamnyeto, Job na wachezaji wengine, naamini tutakuwa mabingwa, ndugu zangu Wazanzibar na Wanayanga wajiandae kushangilia ubingwa,” alisema Bacca.

Yanga walimsajili Bacca wakati wa dirisha dogo la usajili kutokea KMKM, mchezo wao ujao ni dhidi ya Polisi Tanzania unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.