MILANGO ni migumu Uwanja wa Amaan baada ya dakika 45 kumeguka huku ubao ukisoma Simba 0-0 Mlandege FC.
Ni mchezo wa Kombe la Mapinduzi ambapo timu hizi zinasaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.
Jitihada za Simba kuweza kupata bao la kuongoza ndani ya dakika 45 zimegonga mwamba kutokana na nafasi ambazo wamezitengeneza kushindwa kuleta matunda.
Mlandege FC nao jitihada zao za kusaka bao la kuongoza katika mchezo huo kwa kuwa Aishi Manula langoni ameweza kuwa imara.