CHAMA, SIMBA MAMBO SAFI!

AMINI usiamini, sasa ni wazi kuwa zile kelele juu ya usajili wa kiungo mshambuliaji wa RS Berkane, Clatous Chama, zimeisha namna hii, baada ya kuvuja kwa siri ya kwamba tayari Simba imemalizana na mchezaji huyo na tayari wamemrejesha nyumbani kwao Lusaka, Zambia.


Takriban miezi
mitatu sasa, gumzo la jiji ni juu ya usajili wa Chama, ambaye alikuwa mara akihusishwa na Yanga ambao walidhaniwa kumtangazia kitita cha dola laki mbili (200,000), ili avunje mkatabawake lakini sasa upepo wa mchezo umebadilika ghafla baada ya Chama kuvunja mkataba wake chini ya uangalizi wa mabosi wa Simba.


Chanzo
makini kutoka ndani ya Simba, kimelinyetishia Championi Jumamosi kwamba, kelele zote zinazosikika
juu ya Chama ni danganya toto tu,
kwani tayari Chama ameshavuta kitita cha Mohamed Dewji ‘Mo’, ambazo zimemfanya kuvunja mkataba wake na RS Berkane na muda wowote atatua nchini.


“Achana na kelele za mitandaoni,
zaidi naomba uniamini mimi kuwa Yanga hawana uwezo tena wa kumnasa
Chama, maana ishu ilimalizika tangu
Desemba 27, mwaka huu, nchini ya usimamizi wa C.E.O wetu, Barbara
Gonzalez, akiwa sambamba na
aliyekuwa C.E.O wetu wa zamani Crescentius Magori walimaza mchezo mzima.


“Ishu ilikuwa hivi baada ya uongozi
wetu kuona habari zikizagaa juu ya Chama kukosa furaha ndani ya RS Berkane zinazidi kuwa kubwa, ulilazimika kumtafuta na kukaa naye chini ambapo Chama alitaja ukweli kutakiwa na Yanga jambo ambalo walilazimika kuandika barua ya kumuomba kwa waajiri wake hao.


“Hapa ninapokwambia hivi sasa
tayari Chama yupo kwao Zambia akimalizana na familia yake na nina imani kabisa kuwa ndani ya siku mbili zijazo atawasili nchini tayari kwa kuanza majukumu na wenzake baada ya kuachana nao kwa takriban miezi sita iliyopita,” kilisema chanzo hicho.


Championi Jumamosi lilimtafuta
CEO wa Simba, Barbara Gonzalez, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa
haipokelewi hadi tunakwenda
mitamboni.

Stori na Musa Mateja | Championi JUMAMOSI