Home Sports VIDEO:KOCHA SIMBA:AZAM FC INA WACHEZAJI WAZURI

VIDEO:KOCHA SIMBA:AZAM FC INA WACHEZAJI WAZURI

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa Azam FC ni moja ya timu imara na ina wachezaji wazuri hivyo kuelekea kwenye mchezo wao wa kesho Januari Mosi 2022 wanatarajia kupata upinzani mkubwa.

Aidha Pablo amebainisha kwamba ambacho wanahitaji kwenye mchezo huo ni ushindi kwa kuwa maandalizi yameanza kwa muda mrefu na wachezaji wanatambua kwamba wanapaswa kufanya kazi kubwa katika kutoa burudani na kutimiza majukumu yao.

Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zimetoka kushinda mechi zao za mwisho kwa idadi sawa ya mabao ambapo Simba ilishinda mabao 4-1 dhidi ya KMC na Azam FC ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

Previous articleMAYELE NA KAGERE WAPO KWENYE VITA YAO
Next articleNAMUNGO FC YAMPATA MRITHI WA MOROCCO