>

NAMUNGO FC YAMPATA MRITHI WA MOROCCO

KLABU ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imetangaza benchi jipya la ufundi ambalo litainoa timu hiyo kwa msimu wa 2021/22.

Hiyo ni baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Hemed Morocco kuomba kujiweka kando kuinoa timu hiyo kutokana na mwendo ambao haukuwa mzuri kwenye mechi za ligi kwa msimu huu.

Namungo imemtambulisha Hanour Janza ambaye ni raia wa Zambia kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye atakuwa kocha msaidizi.

Anakwenda kufanya kazi na mshambuliaji Relliats Lusajo, Obrey Chirwa pamoja na kiung Shiza Kichuya ambaye aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba.

Mchezo uliopita kwenye ligi Namungo FC ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Biashara United na waligawana pointi mojamoja.