NYOTA wa zamani wa Newcastle Utd, Alan Shearer amesema anaamini wachezaji wa Arsenal wamekubaliana na maamuzi ya kocha wao Mikel Arteta kuhusu kumvua unahodha Pierre Emerick Aubameyang pamoja na kumtoa kwenye mipango yake kwasasa.
“Ilikuwa uamuzi mkubwa na wa kijasiri kutoka kwa Arteta kufanya kile alichokifanya kwa sababu Aubameyang ni nahodha na mshahara ambao analipwa ni mkubwa.
“Lakini lazima aoneshe nidhamu kwa sababu ana timu ya vijana ambayo anajaribu kutuma ujumbe. Sasa wanajua kwamba hawawezi kufanya fujo wala kuchelewa mazoezini.
“Kwa hali hii inaonekana wachezaji wamekubaliana na uamuzi ambao Arteta alifanya kwa sababu wanaonekana tu kwa namna wanavyocheza. Arteta alihitaji wachezaji wake kumuunga mkono katika suala la kumpa kile anachokihitaji kiuchezaji, na wamefanya hivyo kwa mtindo mmoja,” amesema Alan Shearer