NKANE NA YANGA NI SUALA LA MUDA TU

NYOTA wa Biashara United, Denis Nkane na Yanga kwa sasa unaweza kusema kilichobaki ni suala la muda tu kutambulishwa.

Jana alikuwa na kazi ya kupambania timu yake ya Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC na waliweza kugawana pointi mojamoja.

Kwenye mchezo huo ni yeye aliweza kufunga bao la pili na alikuwa anafuatiliwa pia na viongozi wa Yanga wakiongozwa na Injinia Hersi Said.

Ikumbukwe kuwa mtindo huo pia ulitumika kwenye kumalizana na Aboutwalib Mshery ambaye alikuwa akidakia ndani ya Mtibwa Sugar na mchezo wake wa mwisho ilikuwa mbele ya Coastal Union ambapo Mtibwa Sugar ilishinda kwa bao 1-0.

Baada ya mchezo huo Nkane aliweza kusema kuwa anapambana kwa ajili ya timu na kazi yake ni mpira.

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo amemalizana na mabosi wa Yanga hivyo anasubiri kutambulishwa muda wowote kuanzia leo katika usajili wa dirisha dogo ambalo lilifunguliwa Desemba 16 2021 na linatarajiwa kufungwa Januari 15,2022.