JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa anaamini kwamba nyota wake Mohamed Salah atasaini tena mkataba mpya.
Ni miezi 18 imesalia kwa Salah kubaki ndani ya Liverpool ambapo amekuwa akitajwa kwamba anaweza kusepa Anfield.
Ilielezwa kuwa tayari Liverpool wameanza mazungumzo na raia huyo wa Misri ambaye amekuwa na ushkaji mkubwa na kucheka na nyavu kila anapopata nafasi.
Kwa msimu huu wa 2021/22 Salah amefunga jumla ya mabao 22 na asisti tisa kwenye michuano yote.
Kocha huyo amesema:”Tuko kwenye mazungumzo mazuri kabisa, nataka kuona tufanye kila kitu kinakwenda sawa juu yake atasaini hapa,”.