Dnata KUAJIRI WAFANYAKAZI 400,INAFIKA MPAKA ZANZIBAR

    Dnata, kampuni inayotoa huduma za usafiri wa anga na usafirishaji, inatarajia kuajiri zaidi ya wafanyakazi 400 mwezi ujao huko Zanzibar.
    Zanzibar ni sehemu yenye utulivu mkubwa na amani na upendo ni sera ya kiongozi, Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi.
    Kampuni hiyo inayofanya kazi zake katika nchi zaidi ya 30, hivi karibuni ilitangaza kuwekeza dola milioni 7 nchini Zanzibar katika sekta ya anga  na kusimamia shughuli za Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa (T3) cha Abeid Amani Karume (ZNZ) kwa ushirikiano mkubwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na washirika wake.
    Dnata inatarajia kuajiri wafanyakazi wazoefu wa kuhudumia wateja na wamajukumu ya kiofisi na ya kiutendaji, kila moja ikitoa fursa zake za kipekee za maendeleo katika kazi yake.
    Pia kampuni hiyo itatoa ajira katika vyeo mbalimbali kutoka ngazi ya kawaida hadi wasimamizi na usimamizi, kazi zinazohitaji viwango mbalimbali vya uzoefu na elimu.
    Waombaji wa kazi watakaofaulu watasaidia Dnata katika kutoa huduma bora na salama za utoaji huduma za anga, ukarimu katika kuhudumia wateja na usimamizi mzuri wa mizigo na uwanja wa ndege na huduma kwa wateja kwa ujumla katika uwanja wa Abeid Amani Karume wa T3.
    Dnata imejitolea kusaidia watu kufikia uwezo wao wa vipaji na kuwajengea uwezo wa kitaaluma na usimamizi wa talanta na kuwapa  maendeleo yanayofaa ikiwemo  mafunzo na fursa za kazi.
    Dnata ni mojawapo ya watoa huduma wakubwa wa anga duniani. Mshirika anayeaminika wa zaidi ya wateja 300 wa mashirika ya ndege.
    Dnata inatoa huduma za kushughulikia, mizigo, upishi, kushughilikia huduma za usafiri wa anga katika nchi 36. Katika mwaka wa fedha wa 2020-2021  Dnata imeshughulika na ndege zipatazo 290,000, na kuhamisha tani za shehena 2.7milioni , na kuinua milo milioni 17.
    Waombaji wa nafasi mbalimbali za kazi wanaweza kujua zaidi kuhusu majukumu na mahitaji mapya ya Dnata na kutuma maombi ya kujiunga na timu ya kimataifa ya watoa huduma za anga kwenye https://www.emiratesgroupcareers.com/
    Kuhusu Dnata
    Dnata ni mojawapo ya watoa huduma wakubwa wa usafiri wa anga na usafirishaji duniani ilianzishwa mwaka wa 1959.
    Kampuni ya Dnata inatoa huduma za anga na kuhakikisha sekta ya anga inafanya kazi vizuri na kwa ufanisi katika viwanja vya ndege 129.
    Inatoa huduma za usafirishaji, mizigo, usafiri, upishi wa ndege katika nchi 36 katika mabara sita.
    Dnata ni mshirika anayeaminika kwa zaidi ya wateja 300 wa mashirika ya ndege duniani kote. Katika mwaka wa fedha wa 2020-21, timu zinazolenga wateja za Dnata zilishughulikia zamu 280,000 za ndege, kuhamisha tani milioni 2.6 za shehena, kuinua milo milioni 16 na kurekodi jumla ya thamani ya muamala (TTV) ya huduma za usafiri ya dola za Marekani milioni 62.

     

    Previous articleSALAH ATAMWAGA WINO LIVERPOOL
    Next articleYANGA YAMALIZANA NA MASHINE TANO ZA MOTO