TANZIA:-Mama mzazi wa bondia, Hassan Mwakinyo anayejulikana kwa jina la Fatuma Hassan Siri amefariki Dunia Desemba 22.
Alikuwa anasumbulia na tatizo la uvimbe tumboni na alilazwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa muda wa siku sita.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwakinyo aliandika ujumbe huu:”Ama kuna siku nimekosa raha ya kila kitu ulimwenguni ni kukukosa wewe Mlezi wangu,Mama mzazi nilie yatoa maisha yangu kwa utayari wa kufanya kila kitu kwa ajili yako nikulee mzee wangu lakini kwa Mungu haikuwa ridhiki eeh yaaarab nijaalie ustahamilivu msiba wa mama yangu kipenzi, mama yetu.
Pumzika kwa amani mama yetu.
.