KLABU ya Manchester United imeomba Ligi Kuu ya Uingereza kuahirisha mchezo wa leo dhidi ya Brentford baada ya kulazimika kusitisha mazoezi ya kikosi chake cha kwanza Desemba 13 kotokana na Corona.
Kitabu cha mwongozo cha Ligi Kuu ya 2021/22 kinajumuisha itifaki za UVIKO-19, na kinaruhusu bodi ya Ligi Kuu kupanga upya au kuahirisha mechi ya ligi kutokana na sababu za kipekee.
Hatahivyo, kuanzia mechi za leo Jumatano mashabiki wa soka nchini Uingereza watahitajika kuonyesha ushahidi wa kuchanjwa na kutokuwa na maabukizi kuhudhuria mechi yoyote ambapo pia hawapaswi kuzidi mashabiki 10,000.
Vilabu vyote 20 vinavyoshiriki Ligi kuu vimetakiwa kurejea kwenye huduma za dharura ikiwemo kukaa umbali na kuvaa barakoa.