>

NYOTA WATANO SIMBA WATAPIGWA PANGA

SIMBA huenda ikaachana na wachezaji watano mwishoni mwa msimu huu mara baada ya mikataba yao kumalizika,
kati ya hao yupo beki Muivory 
Coast, Pascal Serge Wawa.

Hiyo ni katika kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kitakachofanya vizuri msimu ujao kwenye mashindano mbalimbali. 

Tayari uongozi wa Simba umeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wapyawatakaowasajili.
Mmoja wa mabosi wa Simba, 
ameliambia Spoti Xtra kuwa,  wachezaji hao baadhi wataachwa kutokana na umri mkubwa walionao.


Bosi huyo alisema wachezaji 
hao wamekosa kasi, hivyo Kocha Mkuu, Pablo Franco amependekeza wachezaji hao ambao majina yao yamefichwa kwa sasa.

Aliongeza kuwa, tayari majina hayo kocha ameyakabidhi kwa uongozi, hivyo mwishoni mwa msimu watatangazwa.
“Zaidi ya 
wachezaji watano huenda Simba wakaachana nao mwishoni mwa msimu, kati ya hao yupo Wawa.


“Kwa sasa hapati 
nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, nafasi yake imechukuliwa na Inonga (Hennock) ambaye anacheza kwa kuelewana na Onyango (Joash).

“Wachezaji wengine wanaotajwa ni wale ambao umri umekwenda na hawapati nafasi ya kucheza katika kikosi
cha kwanza,” alisema bosi 
huyo.


Mtendaji Mkuu wa Simba, 
Barbara Gonzalez, hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema:
“Tumepanga 
kufanya maamuzi magumu katika usajili wetu kwa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa watakaofanya vema katika mashindano ya kimataifa.”