Home Sports MO KUTOA BILIONI 2 UJEZI WA UWANJA MPYA

MO KUTOA BILIONI 2 UJEZI WA UWANJA MPYA

MOHAMED Dewji ambaye ni mfanyabiashara na Rais wa Heshima ndani ya Simba  ameahidi kuchangia shilingi za Kitanzania bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Klabu ya Simba.

Mo amesema kuwa ameweza kupokea maoni ya watu wengi ambao ni wadau wa mpira pamoja na mashabiki wa Simba ambao wameweka wazi kwamba wapo tayari kuchangia fedha ili waweze kujenga uwanja mpya.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Mo amesema:-“Nimepokea maoni mengi ya WanaSimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo. Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili.

“Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji. Kwa Kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 billioni. Nawaomba wanasimba tuchange sote,” amesema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba umebainisha namna hii:-“Tunamshukuru Rais wa Heshima wa Simba kufungua milango ya ujenzi wa uwanja wa Simba. Tumeanza mchakato ambao utawezesha Wanasimba kushiriki kuchangia ujenzi. Hivi karibuni tutawatangazia utaratibu,”.

Previous articleKOCHA YANGA AKOSOA MFUMO WA KOCHA MPYA SIMBA
Next articleDROO KURUDIWA 16 LIGI YA MABINGWA ULAYA