KIWA ni saa chache baada ya droo ya kupanga michezo ya hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kufanyika, hatimaye droo hiyo imefutwa na kutangazwa kurudiwa.
Hii inakuja baada ya kutokea kwa tatizo la mfumo unaochezesha droo hiyo na baadhi ya vilabu kulalamikia tatizo hilo.
Awali tatizo lilianza kuonekana pale ambapo Klabu ya Manchester United alipangwa kucheza na Klabu ya Villarreal jambo ambalo halikupaswa kutokea kwani timu hizi mbili zote zilikuwa kundi moja (Kundi F) katika hatua iliyopita ya makundi.
Baada ya kubadilisha, Man United amepangwa kucheza na PSG jambo ambalo limezua utata na kuonesha kuwa kulikuwa na makossa yaliyofanyika awali.
Kupitia ukurasa wao wa Twitter waandaaji wa mashindano hayo wamesema; Kutokana na tatizo hili, matokeo ya droo hii yamefutwa rasmi na droo itarudiwa tena saa 15:00 CET (sawa na 11:00 jioni kwa saa za leo kwa saa za Afrika Mashariki).
Hivi ndivyo timu zilivyokuwa zimepangwa.
⚽Benfica vs Real Madrid
⚽Villarreal vs Man City
⚽Atletico Madrid vs Bayern
⚽FC Salzburg vs Liverpool
⚽Inter Milan vs Ajax
⚽Sporting CP vs Juventus
⚽Chelsea vs Lille
⚽PSG vs Man United.