>

RONALDO AKIWASHA AIPA POINTI TATU MANCHESTER UNITED

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amekiwasha mbele ya kocha mpya wa timu hiyo Ralf Rangnick kwa kufunga bao pekee la ushindi lililoipa timu hiyo pointi tatu.

Ikiwa Uwanja wa Carrow Road, Ronaldo alipachika bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 75 na kufanya ubao usome Norwich City 0-1 Manchester United.

Pointi tatu zinaifanya United kufikisha jumla ya pointi 27 ikiwa nafasi ya tano huku Norwich ikibaki na pointi zake 16 ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Vinara ni Manchester City wenye pointi 38 baada ya kucheza jumla ya mechi 16 wakifuatiwa na Liverpool wenye pointi 37.