>

DAKIKA 45,SIMBA 0-0 YANGA

UWANJA wa Mkapa leo Desemba 11 inachezwa Dabi ya Kariakooo ambapo kwa sasa muda ni mapumziko.

Mpaka dakika 45 za awali zinameguka ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Simba 0-0 Yanga.

mchezo wa leo ushindani ni mkubwa ambapo timu zote zimekuwa zikipambana kusaka ushindi ila milango ni migumu.

Feisal Salum eneo la kati limekuwa mali yake huku utulivu wa Joash Onyango wa Simba ukiweka lango hilo salama kwa sasa.

Ni Onyango pia ameonyeshwa kadi ya njano kipindi cha kwanza baada ya kucheza faulo.