Home Sports IMEISHA HIYO KWA MKAPA, SIMBA 0-0 YANGA

IMEISHA HIYO KWA MKAPA, SIMBA 0-0 YANGA

DAKIKA 90 zimekamilika Uwanja wa Mkapa na ngoma kuwa nzito kwa timu zote ambapo zimegawana pointi mojamoja.

Mpaka mwamuzi wa kazi Herry Sasii anapuliza filimbi ya mwisho kukamilishwa ngwe ya dakika 90 hakuna mbabe kwenye mchezo wa leo.

Yanga inaendelea na rekodi yake ya kucheza mechi ya nane bila kufungwa huku Simba ikiikwama kuivunja rekodi ya Yanga ya kucheza mechi zake bila kufungwa.

Yanga inafikisha pointi 20 nafasi ya kwanza Simba pointi 18 nafasi ya pili.

Yanga ilikuwa imara eneo la kati ikiwatumia Khalid Aucho na Feisal Salum ambaye alikuwa ni mwiba kwa Simba

Simba wao leo walikuwa imara eneo la ulinzi ambapo Mohamed Hussein hakuwa na kazi ndogo ya kufanya.

Joash Onyango ambaye alionyeshwa kadi moja ya njano alikuwa akila sahani moja na Feisal Mayele kwa kusaidiana na Henock Inonga.

Kabla ya mchezo wa leo inaelezwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbra Gonzale aliweza kuzuiwa na maofisa ili asiweze kuingia kwenye mchezo wa leo.

Previous articleDAKIKA 45,SIMBA 0-0 YANGA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI