LEWANDOWSKI KUPEWA TUZO YAKE YA BALLON D’OR

ISHU ya tuzo ya Ballon d’Or imezua sura mpya ambapo kwa sasa inaelezwa kuwa Robert Lewandowski anaweza kupewa tuzo yake ambayo alikuwa anastahili.

Wachambuzi wengi wa masuala ya michezo duniani walikuwa wakihoji kwa nini tuzo hiyo mwaka 2021 iende kwa Lionel Messi licha ya mafanikio makubwa ambayo alipitia Lewandowski.

Lewandowski aliweza kufunga jumla ya mabao 47, 2020 na mabao 64 2021 lakini hana tuzo ya Ballon d’Or.

Kilichomuangusha Lewadowski ilikuwa ni tofauti ya kura 33 ambazo zilimtenganisha na Messi ambaye alipata kura 613 huku yeye akipata kura 580 lakini licha ya Messi kushinda tuzo hiyo bado alitambua mchango wa Lewa.

Messi amesema:”Nadhani unastahili kupewa Ballon d’Or yako.

 “Mwaka uliopita kila mmoja alikuwa anakubali kwamba wewe ulikuwa ni mshindi na nadhani kwamba Shirikisho la Soka la Ufaransa litakupa tuzo yako ambayo ulistahili.

“Nina amini kwamba utakuwa nayo na unapaswa kuwa nayo tuzo yako nyumbani. Wewe ulikuwa ni mshindi halali, (mwaka uliopita)Lakini haikuweza kutokea kwa ajili ya mlipuko wa ugonjwa lakini nina amini kuwa unapaswa kuwa nayo nyumbani,”.