>

AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA KAGERA SUGAR

WAKATI Desemba 9,2021 huu Azam FC ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex Dar,nyota wa kikosi hicho kwenye upande wa utupiaji ameweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu.

Idriss Mbombo,yeye ni mshambuliaji amesema amejipanga kuwamaliza Kagera Sugar kwenye mchezo huo ili kuipa timu yake alama tatu muhimu.

“Kikubwa kuelekea kwenye mchezo wetu maandalizi yapo sawa na tunahitaji kupata pointi tatu ili kuweza kuendelea kwenye kasi yetu ambayo tumeanza nayo.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa kuwa tutakuwa nyumbani na tunachohitaji ni kuona kwamba timu inapata ushindi,”.