>

MANCHESTER UNITED WANATAMBA KITAA KWA USHINDI

Mashabiki wa Manchester United bado wanatamba kitaa kwa ushindi ambao wameupata katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.

Ushindi wa bao 1-0 unawafanya watambe kwa fujo baada ya kusepa na pointi tatu muhimu Uwanja wa Old Trafford.

Bao pekee la ushindi lilipachikwa dakika ya 77 kupitia kwa Fred na kuilaza jumlajumla Crystal Palace na kumfanya Kocha Mkuu wa United Ralf Rangnick kushuhudia kijana wake akishangilia kwa furaha.

Sasa United inafikisha jumla ya pointi 24 baada ya kucheza mechi 15 na Crystal Palace ina pointi 16 ikiwa nafasi ya 13.

Vinara wa ligi ni Manchester City wana pointi 35 wakifuatiwa na Liverpool nafasi ya pili na pointi zao ni 34 wote wamecheza mechi 15.