>

DAKIKA 45,SIMBA YACHEZEWA MPIRA,YACHAPWA KIMOKO

UWANJA wa Mashujaa, nchini Zambia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Red Arrows wanageuza dakika 45 wakiwa ni wababe kwa kuwa wameitungua timu hiyo bao 1-0.

Kasi ya Red Arrows ilianza awali katika dakika 10 za mwanzo na kufanikiwa kupachika bao la kuongoza dakika ya 44.

Ni shuti la mshambuliaji Eric Banda ambaye alitumia mpira wa kurushwa kutoka kwa mchezaji mwenzake kisha akawasoma mabeki ambao walikuwa wakimsindikiza kwa macho alipomtazama Aishi Manula akaachia suti kali likazama nyavuni.

Sasa mzigo unaanza kuwa mzito kwa Simba kwa kuwa Pablo Franco ameonekana kuwapa mbinu za kujilinda wachezaji wake.