LICHA ya Mohamed Salah, raia wa Misri kukosa tuzo ya Ballon d’Or iliyokwenda kwa Lionel Messi raia wa Argentina anayekipiga ndani ya PSG,nyota huyo nali ya Liverpool ameendelea kukiwasha.
Katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-1.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Henderson dakika ya 9 huku Salah akitupia mabao yake dakika ya 19 na 64 bao la nne lilipachikwa na Jota dakika ya 79.
Lile la Everton lilifungwa na Gray dakika ya 38 katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Matokeo mengine ilikuwa ni Watford 1-2 Chelsea hivyo gari kwa Chelsea unaweza kusema limewaka.