SAID Ntibanzokiza, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kuelekea katika mchezo wao wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba wapi tayari.
Kiungo huyo alianza katika kikosi cha kwanza kulichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza ameanza kuingia kwenye mfumo wa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi.
Katika mabao hayo mawili nyota huyo alifungua akaunti ya mabao kwa kupachika bao moja kwa pigo huru akiwa nje ya 18 iliyomuacha kipa wa Mbeya Kwanza, wazee wa kinyumenyume akiwa hana chaguo.
Desemba 11, Yanga inatarajiwa kuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Simba mchezo utakaopigwa Uwanja wa Mkapa.
Nyota huyo amesema:”Tumemaliza kazi mchezo wetu uliopita sasa ni muda wa kuanza kufanya maandalizi kwa mchezo wetu ujao dhidi ya Simba.
“Haitakuwa kazi rahisi tutapambana kufanya vizuri ili kupata matokeo chanya kwa kuwa wachezaji wote tupo tayari na mwalimu pia tuna amini atatupa kile ambacho ni bora zaidi,”.