WAKATI Arsenal wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho kwa sasa kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United kuna hatihati ya kuweza kukosa huduma ya nyota Bukayo Saka.
Licha ya matumaini kuwa makubwa bado mpaka sasa haijathibitishwa kwamba nyota huyo anaweza kucheza ama la mbele ya Manchester United.
Ikumbukwe kwamba Saka ambaye amekuwa ni chachu ya ushindi kwa Arsenal aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United wakati Arsenal iposhinda mabao 2-0 ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Ripoti zinaeleza kuwa ni tatizo la msuli ambalo lilimsumbua kijana huyo ambaye amekuwa akionyesha uwezo mkubwa uwanjani.
Kesho, Uwanja wa Olld Trafford utapigwa mpira mkubwa sana kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal ambao ni wa Ligi Kuu England.