>

CR 7 AWAKA KISA BALLON d’OR

CRISTIANO Ronaldo, nyota wa kikosi cha Manchester United ametoa ujumbe wenye hasira kuhusu Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia, (Ballon d’Or) baada ya mpinzani wake Lionel Messi kushinda.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United amemshutumu bosi wa Ballon d’or Pascal Ferre aliyetamka kuwa ndoto kubwa ya Ronaldo ni kumaliza maisha yake ya soka akiwa na tuzo hizo nyingi zaidi ya Messi.

Ni nafasi ya sita Ronaldo alimaliza kwenye halfa ya tuzo hizo ambazo zilitolewa juzi na Messi alitwaa tuzo yake ya saba.

Ikumbukwe kwamba Ronaldo wala hakuweza kuhudhuria tuzo hizo ambazo zimekuwa na malalamiko kadhaa kutokana na ushindi wa nyota huyo.

Kwenye ukurasa wake wa Insta,Ronaldo aliandika:”Kilichotokea leo, (juzi) kinaelezea matamshi ya Pascal Ferre wiki iliyopita aliposema kuwa lengo langu pekee ni kumaliza maisha yangu ya soka nikiwa na tuzo nyingi zaidi ya Lionel Messi.

“Pascal Ferre alidanganya, alitumia jina langu kujitangaza na kulitangaza gazeti analofanyia kazi. Haikubaliki mtu anayehusika kutoa tuzo ya namna hiyo kudanganya kwa kiwango hicho.

“Nataka kuwapongeza wote walioshinda, nacheza bila kushindana na yeyote,”.