>

DAKIKA 45, SIMBA YAENDA MAPUMZIKO KIFUA MBELE

UWANJA wa Mkapa leo mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Geita Gold tayari dakika 45 zimekamilika.

Simba inakwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao moja kwa bila ambalo limefungwa na Peter Banda.

Ilikuwa ni dakika ya 9 baada ya Simba kuanza kwa kasi kuliandama lango la Geita Gold ambao dakika tano za mwanzo walianza kuliandama lango la Simba.

Ni pasi ya Kibu Denis iliweza kutumiwa vema na Banda ambaye hakufanya makosa kupachika bao hilo kimiani.

Geita Gold sio watu wa kubeza kwa kuwa wamekuwa imara katika kuzuia mashambulizi ya Simba na wamefanya jitihada kubwa ndani ya dakika 45.

Juma Mahadhi amekuwa ni mwiba kwa Simba ambapo Aishi Manula alikuwa akifanya jitihada kutimiza majukumu yake katika kufanya kazi ya kuokoa michomo.

Inaonekana kwamba mabeki wa Simba bado hawana utulivu huku nyota wa mchezo mpaka sasa kwa Simba akiwa ni Banda.

Ibrahim Ajibu amekosa utulivu ambapo kwenye pasi ano ambazo ametoa hakuna ambayo imeweza kumfikia mlengwa na Geita Gold tayari gari limewaka.