NYOTA wa kikosi cha PSG, mshambuliaji Lionel Messi mambo kwake ni magumu kwenye ishu ya kucheka na nyavu baada ya kuweka rekodi ya kucheza mechi tano bila kufunga.
Ni giza nene limeendelea kutanda kwenye macho yake kwa sasa staa huyo ambaye alikuwa akikiwasha ndani ya Barcelona kwani tayari amecheza mechi hizo ndani ya Ligue 1 bila kucheka na nyavu.
Mbele ya Lille pia Messi alishindwa kuwaka wakati timu yake ikishinda mabao 2-1 alitolewa uwanjani baada ya kuumia.
Nyota huyo ndani ya Ligue 1 ametumia jumla ya dakika 325 bila kufunga wala kutoa pasi ya bao na alipokuwa ndani ya Barcelona alitupia jumla ya mabao 30 na alisepa na tuzo ya mfungaji bora.