Home Sports MABINGWA WATETEZI WABANWA MBAVU KWA MKAPA

MABINGWA WATETEZI WABANWA MBAVU KWA MKAPA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo Oktoba 31 wamebwana mbavu mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kugawana pointi mojamoja.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wa nguvu nyingi imeshuhudiwa ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-0 Coastal Union ya kule Tanga.

Kadi mbili nyekundu leo zimetolewa ambapo kila timu imeonyeshwa kadi moja nyekundu ni Benedict Mwamlangala wa Coastal Union huyu alionyeshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo wa leo na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Ni beki kisiki wa Simba, Henock Inonga ambaye alifanya kazi yake vizuri mwanzo, mwisho akaharibu dakika ya 90 kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonekana akimpiga kichwa mchezaji wa Coastal Union.

Licha ya washambuliaji wake watatu kupata nafasi ikiwa ni pamoja na nahodha John Bocco, Kibu Dennis na Meddie Kagere walikwama kutupia kwenye mchezo wa leo.

Previous articleMESSI MAMBO MAGUMU PSG
Next articleYANGA MACHO KWENYE UBINGWA WA LIGI KUU BARA