Home Sports YANGA MACHO KWENYE UBINGWA WA LIGI KUU BARA

YANGA MACHO KWENYE UBINGWA WA LIGI KUU BARA

BAKARI Mwamnyeto,  nahodha wa Yanga amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

 

Yanga ikiwa imecheza mechi nne imeshinda zote na kujiwekea kibindoni pointi zake 12 inashika nafasi ya kwanza huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 6.

Wapinzani wao Simba wapo nafasi ya nne na pointi 8 baada ya kucheza mechi nne huku safu ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao mawili.

Mwamnyeto amesema:”Ligi ni ngumu hilo tunajua lakini tunahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa ni malengo yetu na inawezekana, “.

Previous articleMABINGWA WATETEZI WABANWA MBAVU KWA MKAPA
Next articleHUU HAPA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU