OLE MBISHI KINOMANOMA ATAJA SABABU ZA KUBAKI UNITED

OLE Gunnar Solkajaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa ametoka mbali na timu hiyo jambo ambalo linamfanya azidi kubaki ndani ya timu hiyo.

Kocha huyo hakuwa na bahati alipokutana na Liverpool na alishuhudia ubao wa Uwanja wa Old Trafford ukisoma Manchester United 0-5 Liverpool ikiwa ni kipigo kikubwa kwa timu hiyo kwa msimu wa 2021/22 kutoka kwa Liverpool.

Wachambuzi na mashabiki wamekuwa wakieleza kuwa tayari muda wa kocha huyo kusepa umefika huku jina la Antonio Conte likitajwa kubeba mikoba yake ili aweze kumaliza mwendo ndani ya Ligi Kuu England jambo ambalo linatajwa kuwa ni la muda tu kwake kuondoka.

Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu kipigo hicho cha mabao matano ambapo wengi wanasema kuwa sio kipigo cha kawaida bali ni kipigo cha udhalilishaji na Solskjaer amesema kuwa ametoka mbali na timu hiyo.

“Nimetoka mbali na timu hii, kama kundi tumetoka mbali sana na tunakaribia kuachana sasa. Nafikiri siwezi kusema tofauti na kile ambacho kimetokea.

“Ni ngumu kucheza na Liverpool na kuwapa nafasi zote zile lakini ajabu ni kwamba sisi tulifanya hivyo kiwango chetu hakikuwa sahihi kabisa,”.