Home International NGUMU KUMFANANISHA SALAH NA RONALDO

NGUMU KUMFANANISHA SALAH NA RONALDO

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool ambaye anaamini kwamba nyota wake Mohamed Salah ni moja ya wachezaji bora kwa sasa duniani ila ni ngumu kumfananisha na Cristiano Ronaldo ambaye anakipiga ndani ya Manchester United.

Miamba hao wawili wanakiwasha ndani ya Ligi Kuu England huku ile safu ya ushambuliaji ya Liverpool ikiwa ni namba moja kwa utupiaji ikiwapoteza wale wa Manchester United.

Katika mechi za tisa za Ligi Kuu England, Liverpool imetupia jumla ya mabao 27 huku safu yao ya ulinzi ikiwa imeokoteshwa mabao 6 pekee katika nyavu zao.

Hapo kwa rekodi inaonekana kwamba Liverpool wana jambo lao hasa inapokuja katika suala la kufunga kwenye ligi hiyo pendwa duniani huku Manchester United mambo yakiwa magumu.

Ukitazama rekodi za United wao safu yao ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 16 na imeruhusu mabao 15 katika mechi 9 jambo linalompasua kichwa Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer namna atakavyokwenda sawa na vijana hao.

Tegemeo lao katika safu ya ushambuliaji ndani ya United ni Ronaldo mwenye mabao matatu huku wengine ambao wanafanya poa ni Bruno Fernandes na Mason Greenwood ambao wametupia mabao mannemanne kila mmoja.

Mkali wa pasi za mwishi ni kiungo wao mkorofi, Paul Pogba ambaye ametoa jumla ya pasi 7 raia huyo wa Ufaransa akiwa ni mtengeneza mipango namba moja.

Kwa Liverpool wao namba moja ni Salah mwenye mabao 10 na pasi aliwatungua hat trick United walipokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England huku Sadio Mane yeye akiwa ametupia mabao matano ndani ya Ligi Kuu England

Previous articlePOLISI TANZANIA YAWAPIGA MKWARA MABINGWA
Next articleUSALITI WATAJWA ISHU YA KIPIGO CHA SIMBA