Home Sports POLISI TANZANIA YAWAPIGA MKWARA MABINGWA

POLISI TANZANIA YAWAPIGA MKWARA MABINGWA

UONGOZI wa Polisi Tanzania umeweka wazi kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Oktoba 27 wataendelea pale ambapo wameishia kwa kucheza pira chukuchuku ili waweze kusepa na pointi tatu muhimu.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi tisa kibindoni baada ya kucheza mechi tatu na kutupia mabao matano wanafuatiwa na Yanga walio nafasi ya pili na pointi tisa ikiwa imetupia mabao manne.

Inatarajiwa kukutana na mabingwa watetezi wa ligi ambao wametoka kunyooshwa kwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy jana Uwanja wa Mkapa na kufungashiwa virago kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa wapo ndani ya Kombe la Shirikisho.

Jana Polisi Tanzania ilisepa na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ikiwa ugenini Uwanja wa Mabatini na kuwafanya waweze kucheza jumla ya mechi tatu bila kupoteza.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma ameweka wazi kuwa maandalizi yanakwenda vema na vijana wapo tayari kwa ajili ya ushindani.

Kinara wa utupiaji kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara ni Vitalis Mayanga ambaye alipachika bao lake la tatu kwa kuwatungua Ruvu Shooting, Uwanja wa Mabatini.

Previous articleMWIJAKU AHADI YAKE MPAKA MWANASHERIA
Next articleNGUMU KUMFANANISHA SALAH NA RONALDO