SIMBA YAMTANGAZA WAZIRI WA MAJI MGENI RASMI DHIDI AL AHLY LEO
Klabu ya Simba imemtangaza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuwa mgeni rasmi wa mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly utakaochezwa leo Machi 29, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 3 usiku. Huu ni mchezo wa kwanza kwa Simba ambao wanahitaji matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya…
SIMBA HESABU KIMATAIFA KUONGEZA DOZI, AL AHLY KUTUA LEO
BENCHI la ufundi la Simba limebainisha kuwa litawaongezea dozi wachezaji wao kwenye uwanja wa mazoezi kuwa imara zaidi katika mechi wanazocheza ikiwa ni pamoja na safu ya ulinzi. Ipo wazi kwamba ndani ya Ligi Kuu Bara, safu ya ulinzi ya Simba imekuwa na mwendo mbovu katika ulinzi ndani ya timu tatu zilizo kwenye tatu bora…
MWAMBA CLATOUS CHAMA MDOGOMDOGO ANAJITAFUTA
MWAMBA wa Lusaka Clatous Chama anajitafuta ndani ya Simba akirejea kwenye ubora wake taratibu akiwa ni kinara wa pasi za mwisho za mabao msimu wa 2023/24 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na wamefunga mabao 39 ndani ya Ligi Kuu Bara
YANGA HAINA HOFU NA MAMELODI KWAO AMANI TU
UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba hauna tatizo na wapinzani wao kwenye anga la kimataifa Mamelodi Sundowns kwa kuwa vita yao ni ndani ya dakika 90 uwanjani. Yanga wameweka wazi kuwakama kuna mashabiki wao ambao wapo Tanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kikubwa ni kuona wanapata burudani kwenye mchezo huo wa kimataifa unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa….
SIMBA; MASHABIKI KUFIKA UWANJANI NI MATENDO YA LAZIMA
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa miongoni mwa matendo ya lazima kwa mashabiki wa Simba ambao wana afya njema na mapenzi na timu hiyo ni kufika uwanjani Machi 29 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mkapa hatua ya robo…
ANATUA USIKU MNENE MTU WA KAZI YANGA KUWAKABILI MAMELODI
KUELEKEA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns, uongozi wa Yanga umebainisha kwamba upo tayari kwa mchezo huo na wachezaji wake watawasili Tanzania muda wowote hata usiku wa manane kuwakabili wapinzani wao. Mchezo wa Yanga dhidi ya Mamelodi unatarajiwa kuwa Machi 30 2024 Uwanja wa Mkapa ikiwa ni hatua…
SIMBA YAKAMILISHA KAMBI SASA KAMILI KUWAVAA AL AHLY
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wamewasili Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly. Kikosi cha Simba Machi 19 kiliweka kambi Zanzibar kwa ajili ya kambi maalumu ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly. Mchezo huo…
YANGA: USHINDI WETU KIMATAIFA TUNALIHESHIMISHA TAIFA
KUELEKEA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns, Yanga wameweka wazi kuwa ushindi wao unakwenda kuliheshimisha taifa la Tanzania kwenye anga la kimataifa. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 30 2024 Uwanja wa Mkapa ambapo kiingilio mzunguko ni bure.
SIMBA YAIATAKA NUSU FAINALI, KUBADILIKA NA AL AHLY
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa umechoka kuishia hatua ya robo fainali mara kwa mara hivyo safari hii katika Ligi ya Mabingwa Afrika mpango mkubwa ni kutinga nusu fainali na wataanza kupambana na Al Ahly kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Machi 29 Uwanja wa Mkapa
AZAM FC YAREJEA CHIMBO
KIKOSI cha Azam FC kinachofundishwa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo kimerejea chimbo kwa maandalizi ya mechi za ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara. Azam FC inaingia kwenye rekodi ya timu mbili ambazo zimepata ushindi mbele ya Yanga inayofundishwa na Miguel Gamondi katika mechi za ligi. Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wamekuwa kwenye mwendo bora…
SIMBA YAPIGA HESABU NDEFU KWA AL AHLY KIMATAIFA
UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba hesabu kubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zote mbili za kimataifa hatua ya robo fainali kwa kuanza na kazi Uwanja wa Mkapa dhidi ya Al Ahly ya Misri. Ipo wazi kwamba Al Ahly watakuwa wapinzani wa Simba kwenye hatua ya robo fainali wakipata ushindi dhidi yao watatinga nusu fainali kwenye…
HII HAPA SIRI YA MWAMBA AZIZ KI
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Aziz KI raia wa Burkina Faso ameweka wazi kuwa ushirikiano mkubwa kutoka kwenye benchi la ufundi pamoja na wachezaji ni nguzo kubwa kupata mafanikio katika mechi wanazocheza. Ipo wazi kwamba Aziz KI ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga akiwa na mabao 13 idadi hiyo ni sawa na kiungo wa Azam…
TAIFA STARS YAPETA KIMATAIFA
HATIMAYE timu ya taifa ya Tanzania imepeta kimataifa kwa kupata ushindi kwenye mchezo wake wa pili ikiwa ugenini. Ikumbukwe kwamba katika LS
KIMATAIFA YANGA NI MUDATHIR YAHYA
UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns itakuwa ni siku ya simu kuita kwa kuwa mchezo utakuwa kwenye miguu ya Mudathir Yahya. Yahya chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Miguel Gamondi amekuwa kwenye mwendelezo bora katika mechi za Ligi Kuu Bara ambapo mtindo wake wakushangilia pale…
VIDEO; JEMBE: ISHU YA BURE YANGA KUNA TATIZO MAHALI
LEGEND kwenye masuala ya uandishi wa Habari za Michezo kitaifa na Kimataifa Bongo, Saleh Ally, (Jembe) ameweka wazi kuwa kuna mahali haipo sawa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundonws baada ya mabosi Yanga kubainisha kuwa mzunguko itakuwa ni bure.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 30 2024 Uwanja wa…