
CHAMA, SIMBA MAMBO SAFI!
AMINI usiamini, sasa ni wazi kuwa zile kelele juu ya usajili wa kiungo mshambuliaji wa RS Berkane, Clatous Chama, zimeisha namna hii, baada ya kuvuja kwa siri ya kwamba tayari Simba imemalizana na mchezaji huyo na tayari wamemrejesha nyumbani kwao Lusaka, Zambia. Takriban miezi mitatu sasa, gumzo la jiji ni juu ya usajili wa Chama,…