
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne, nakala yake ni jero tu
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne, nakala yake ni jero tu
WILFRED Kidao Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF ) amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya DR Congo yapo vizuri na wanaamini kwamba watafanya vizuri katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 11,2021, Stars ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya DR Congo katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapaa saa…
Aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Hitimana Thierry, amevunja ukimya na kutaja kuwa kukamiwa na kuchezewa kwa nguvu nyingi na wapinzani wao ndiyo chanzo kikubwa cha wao kupata kadi nyekundu kwenye mechi wanazocheza nao. Hitamana ametoa kauli hiyo kufuatia kutokea kwa kadi nne nyekundu walizopewa wapinzani wao katika mechi nne kati ya tano walizocheza mpaka sasa kwenye ligi kuu. Katika mchezo wa pili dhidi ya Dodoma Jiji, ilitoka kadi nyekundu ya kwanza…
MKURUGENZI wa Uwekezaji wa GSM na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema mjadala ulioanzishwa na baadhi ya wachambuzi kuhusu udhamini wa kampuni ya GSM kwa vilabu mbalimbali ligi kuu ni siasa chafu kwa kuwa sio jambo geni katika ulimwengu wa soka. Akizungumza na EA Radio, Injinia Hersi amesema…
MABOSI wa Simba na Yanga kwa sasa ikiwa watakuwa wanahitaji kupata saini ya beki wa kazi ndani ya kikosi cha Azam FC,Daniel Amoah lazima wajipange kwa kuwa amejifunga miaka mingine zaidi. Novemba 4, Amoah ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, George Lwandamina aliongeza dili la miaka miwili hivyo ataendelea kuwa ndani ya Azam…
UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa wachezaji wote ambao wamesajiliwa na kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22 ni vyuma vya kazi jambo ambalo linawapa tabu benchi la ufundi kwenye suala la upangaji wa kikosi. Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi 15 huku safu yao ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao tisa na ile ya ulinzi imeokota…
SIMULIZI ya kijana aliyefanya makosa wakati wa kutuma shilingi, mkwanja kwa ndugu yake na namna muamala wake ulivyoweza kurejea. Sijawahi kuhisi jinsi nilihisi wakati mtu mmoja kwa jina Mpapale alipokea pesa yangu na kukataa kuirudisha. Nilikuwa na mgonjwa katika Hospitali moja kubwa Afrika Mashariki na ilipangwa kutolewa Ijumaa. Nilikuwa nimepata mshahara wangu na nilidhani ni…
UWANJA wa London mambo yalikuwa magumu kwa Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England baada ya kutulizwa kwa kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Westham United. Atajilaumu Alisson Ramses Becker ambaye alijifunga dakika ya nne katika harakati za kuokoa kona kisha Pablo Fornals alipachika kamba ya pili dakika ya 67 na msumari wa ushindi ulipachikwa…
MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingiza, ameweka wazi mpango mkakati wa kuhakikishatimu yao inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ni kuuchukulia kila mchezo kama fainali jambo ambalo litawanufaisha zaidi kukusanya pointi katika michezo yao. Yanga mpaka sasa wanaongoza ligi kuu wakiwa na pointi 15 baada ya kufanikiwa kushinda michezo yote mitano, wakiwa wamefunga mabao tisa na kuruhusu moja. Senzo amesema ukubwa wa Yanga ndio chanzo cha kuhitaji kutwaa ubingwa…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Novemba 7 kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za kimataifa za kufuzu Kombe la Dunia. Mchezo ujao kwa Stars ni dhidi ya DR Congo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa soka Bongo. Utachezwa Novemba 11,2021, Uwanja wa…
RAMADHAN Nswazurimo, Kocha Mkuu wa Klabu ya DTB amesema kuwa wachezaji wake waliamini wameshinda kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ken Gold jambo lililowafanya wapate tabu ndani ya dakika 90. Mchezo wa leo wa Championship uliochezwa Uwanja wa Uhuru ulikuwa na ushindani mkubwa na timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu. Mwisho wa siku ushindi…
MEDDIE Kagere ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu wa 2021/22 ameshindikana kwa kuwa ni kinara wa mabao akiwa nayo mawili na amefunga yote akitokea benchi na kumfanya afikishe jumla ya mabao 60 ndani ya Ligi Kuu Bara tangu aanze kucheza Bongo. Kagere aliyeibuka ndani ya Simba msimu wa 2018/19, bao lake la kwanza kwa msimu wa 2021/22 alipachika mbele ya Dodoma Jiji akitumia pasi ya mshikaji wake Chris Mugalu na alifunga akitoka…
MKURUGENZI wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo ametoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya vilabu vya soka nchini kubadili nembo za wadhamini kwenye jezi zao. Nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu Bara NBC ina rangi nyekundu jambo ambalo halikubaliki kwa Yanga kwa mujibu wa katiba yao jambo ambalo limepelekea wao kubadilishiwa nembo na kuvaa twiga mwenye rangi…
Real Madrid imetajwa kuwa ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota wa Chelsea, Antonio Rudiger ambaye ni beki wa kati. Ikiwa dili lake litajibu basi mkwanja ambao atalipwa kwa wiki itakuwa ni pauni 200,000 na ni itakuwa kwa wiki jambo ambalo linaongeza urahisi katika kukamilisha dili hilo. Madrid ipo tayari kuwauza wachezaji wake…
MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya YANGA, Eng Hersi Said amesema amepata tetesi za viongozi wa klabu ya Simba hivi karibuni kuonekana mara kadhaa nyumbani kwa wazazi wa beki kinda wa Yanga Kibwana Shomari. “Ninazo taarifa hizo kupitia mchezaji mwenyewe na watu wangu wa karibu kuhusu ziara zenye nia ya kumshawishi…
Muonekano wa gazeti la Spoti Xtra Jumapili lipo mtaani nakala yake ni 500.