Home Sports SIMBA KUIKABILI NAMUNGO WAKIWA NA HOFU

SIMBA KUIKABILI NAMUNGO WAKIWA NA HOFU

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo Mei 3 wana kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Namungo huku wakiwa na hofu kuhusu mchezo wa leo.

Mchezo huo ni wa ligi ikiwa ni mzunguko wa pili ambapo wababe hao wanatarajiwa kuwa kwenye msako wa pointi tatu kama itakavyokuwa kwa Namungo.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza Simba ilishinda bao 1-0 hivyo leo ina kibarua kingine kuweza kusaka ushindi mbele ya Namungo ambayo imezidi kuwa imara.

Pablo Franco Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anawatambua Namungo kwa kuwa walimpa tabu kwenye Kombe la Mapinduzi.

“Ninaikumbuka Namungo nilikutana nayo kwenye Kombe la Mapinduzi nikashinda lakini haikuwa rahisi hivyo tutajitahidi kupata ushindi,”

Simba imetoka kugawana pointi mojamoja mbele ya Yanga huku Namungo FC ikitoka kuibamiza mabao 3-1 Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Ilulu.

Kwenye msimamo Namungo FC ipo nafasi ya 3 ikiwa na pointi 29 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 42.

Kikosi cha Simba jana kilifanya mazoezi ya mwisho na miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye hesabu za mwisho ni Henock Inonga,Mzamiru Yassin na Rally Bwalya.

Previous articleKIBWANA,SAIDO BADO HAWAJAPEWA MIKATABA
Next articleYANGA KUINGIA KAZINI KWA MARA NYINGINE TENA